Thursday, July 23, 2020

Zitto Aweka Wazi Idadi Ya Wanachama ACT “Tunaizidi CCM”

Maalaim Seif Mwenyekiti mpya ACT-WazalendoKiongozi mkuu wa chama ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amesema chama hicho kina wanachama wengi zaidi kuliko chama tawala cha mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar tofauti na wakati kinapoanzishwa chama hicho miaka sita iliyopita.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum na mwandishi wa habari mkongwe nchini Jenerali Ulimwengu, akiongelea juu ya ukuaji wa chama hicho kilichoanza kikiwa na mbunge mmoja tu kwenye bunge lilopita.

“Kwa sasa jumla ya kadi tulizozitoa ni milioni moja na kitu kwa Zanzibar tuna jumla ya wanachama laki mbili na kidogo..tuna wanachama wengi zaidi Zanzibar kuliko CCM kwenye rekodi CCM ina wanachama 160,000 sisi tuna wamchama 230,000 kwa hiyo tuna chama kikubwa kinachokuwa kwa kasi sasa hivi” amesema Zitto.

Chama cha ACT kilianzishwa rasmi mwaka 2014 na kilishiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, huku kikifanikiwa kushika nafasi ya tatu kwenye matokeo ya jumla wa urais na kupata kiti kimoja cha ubunge na madiwani kadhaa.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/23/zitto-aweka-wazi-idadi-ya-wanachama-act-tunaizidi-ccm/

No comments:

Post a Comment