Rais John Magufuli amefika msibani Masaki jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuyka pole kwa familia ya marehemu Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa.
Rais Magufuli amesaini kitabu cha maombolezo cha Hayati Benjamin Mkapa.
Rais Mstaafu Mkapa amefariki jana kuamkia leo alipokuwa amelazwa hospitali kwa ajili ya matibabu jijini Dar es Salaam.
JPM alipofika msibani Masaki Jijini Dar es Salaam na kutia saini kitabu cha maombolezo ya Hayati Benjamin William Mkapa (Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu). pic.twitter.com/7rmpwMFB5C
— Gerson Msigwa (@MsigwaGerson) July 25, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amefika msibani Masaki Dar es salaam ambapo amesaini kitabu cha maombolezo na kutoa pole kwa familia ya Marehemu Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa.#RIPMkapa pic.twitter.com/FJTqdVHBy3
— EastAfricaRadio (@earadiofm) July 25, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/07/25/rais-magufuli-awasili-msibani-na-kutoa-pole-kwa-familia-ya-mkapa/
No comments:
Post a Comment