Friday, July 31, 2020

Bingwa wa Ndondi Mayweather kurudi Uwanjani Baada ya Kustaafu, Uhondo Kamili

Floyd Mayweather: Khan claims ex-boxer will come out of retirement because he's broke

Huenda Mayweather atarejea uwanjani mwaka huu

Bingwa huyo wa ndondi anadaiwa kumaliza hela zote alizowehifadhi

Mwanandondi mwenza Amir Khan ametoa madai hayo

Aliyekuwa nyota wa ndondi Floyd Mayweather atarejea uwanjani mwaka huu kwa mara ya kwanza tangu alipostaafu 2017, hii ni kulingana na mwanandondo mwenza Amir Khan.

Mayweather aliyestaafu 2017 akiwa na umri wa miaka 40 anadaiwa kuchukua hatua ya kurejea kwenye uwanja baada ya kufyonza fedha zote alizowekeza huku sasa umaskini ukimkodolea macho.

Floyd alitengeneza mabilioni ya pesa baada ya kuibuka mshindi kwa takriban mechi 50 alizoshiriki mtawalia na kuibuka mshindi.

‘’ Floyd Mayweather ni kati ya wale ambao huenda wamemazliza hela zao na watalazimka kurudi uwanjani,’’ Amir Khan alisema.

Anatumia hela nyingi sana, ila sijui kama atapenda wazo hilo la kurudi uwanjani. Kama nilivyosema, huenda atarudi,’’ aliongezea.

Inadaiwa kuwa Floyd alikuwa akipata mshahara mrefu wa  $1 bilioni lakini Mc Gregor pamoja na aliyekuwa rafikiye wa karibu 50 Cent alifyonza hela hizo zote.

Iwapo atarudi uwanjani, Mayweather ataibua kibarua kigumu kwa wanandondi wenza maana hamna aliyefanikiwa kumpiku katika mchezo huo.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/31/bingwa-wa-ndondi-mayweather-kurudi-uwanjani-baada-ya-kustaafu-uhondo-kamili/

No comments:

Post a Comment