Friday, July 24, 2020

Benjamin Mkapa:  Viongozi wa Afrika Waungana na Watanzania Kumuomboleza Aliyekuwa Rais Wao

Former Tanzania's President Benjamin Mkapa dies in hospital aged 81

Benjamin Mkapa alifariki alipokuwa akipata matibabu katika hospitali moja jijini Dodoma, Ijumaa, Julai 24. Picha: Hisani

Kifo chake kilitangazwa na Rais wa Jamhuhuri ya Tanzania Johhn Pombe Magufuli akitangaza siku saba za kumuomboleza

Moussa Faki, aliyekuwa mwenyekiti wa  AUC, Rais Uhuru Kenyatta, Raila Odinga, Yoweri Museveni ni kati ya viongozi waliomuomboleza

Viongozi kote Afrika wameungana na jamuhuri ya Tanzania katika kumuomboleza aliyekuwa rais wa nchi hiyo Benjamin Mkapa aliyefariki Ijumaa, Julai 24 hospitalini alikokuwa akipata matibabu.

Habari kuhusu kifo chake kilitangazwa na Rais John Pombe Magufuli katika idhaa ya taifa ya TBC huku akitangaza kuhusu siku saba ya maombolezi.

Viongozi wa Afrika wamejitokeza kwa kila njia kumuomboleza  kiongozi huyo kwa kutuma jumba za rambi rambi  kwa ndugu jamaa na marafiki.

Aliyekuwa mwenyekiti wa muungano wa AUC, Moussa Faki Mahamat alimtaja hayati Benjamin Mkapa kama mweka Amani mkuu katika eneo la Afrika Mashariki.

‘’Ni kwa huzuni kubwa, nimepata kujua kuhusu kifo cha Mzee Benjamin Mkapa, aliyekuwa Rais wa Tanzania,’’ Mousa aliandika.

Mzalendo anayekumbukwa haswa kwa kuwa mweka Amani Afrika Mashariki. Maombi yangu yaendee familia, Watanzania pamoja na serikali ya Tanzania,’’ aliongezea.

Rais Uhuru Kenyatta alimtaka hayati Mkapa kama mdumishi wa Amani na aliyefanya kila nia kupigisha Afrika mashariki hatua nyingi.

Aliyekuwa Waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga alimkumbuka Mkapa kama rafiki mkuu wa Kenya na mzalendo wa ajabu.

Kifefe Kizza Besigye naye hakuachwa nyuma, Mtetezi mkuu wa haki za kibinadamu Uganda alimtaja Mkapa kama kiongozi aliyeacha kumbukumbu wa huduma na uadilifu mkubwa.

Viongozi wengine walioungna na Jamuhuri ya Tanzania katika kumuomboleza kiongozi wao ni pamoja na wabunge, maseneta na viongozi mbali mbali mbali.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/24/benjamin-mkapa-viongozi-wa-afrika-waungana-na-watanzania-kumuomboleza-aliyekuwa-rais-wao/

No comments:

Post a Comment