Alipata fununu kuwa bintiye huyo mwenye umri wa miaka 16 alikuwa na mpenzi mtaani humo
Alimchoma kwa pasi makalio kabla kugeukia sehemu nyeti
Msichana huyo alilazwa hospitalini kwa majeraha mabaya
Polisi katika kaunti ya Bungoma, Kenya wameanzisha msako mkali dhidi ya jamaa anayedaiwa kumchoma bintiye mwenye umri wa miaka 16 sehemu nyeti.
Jamaa huyo anadaiwa kutekeleza unyama huo katika kijiji cha Bukembe kaunti ndogo ya Kanduyi kabla kutoweka.
Kulingana na ripoti ya polisi, kisa hicho kiliripotiwa na mama wa binti huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya upili ya Bukembe SA.
Maafisa wa polisi wameanzisha msako dhidi ya mshukiwa huyo. Picha: Hisani.
Baba huyo alichukua pasi na kumchoma mwanawe makalio kabla kumchoma hadi sehemu ya siri.
Akizungumza katika hospitali ya rufaa ya Bungoma akilolazwa, msichana huyo alilalamika kuhusu maumivu makali huku akishangaa kuhusu kilichomfanya babake kumfanyia unyama huo.
‘’ Nashangaa ni kwanini napitia haya,’’ alisema kwa maumivu makuu.
Kulingana na mamake mwanadada huyo, babake alipata fununu kutoka kwa majirani kuwa bintiye alikuwa akiishi na jamaa mwengine mtaani humo.
Akithibitisha kisa hicho, OCPD wa Bungoma Wilson Nanga alieleza kuwa msichana huyo alitibiwa katika zahanati moja mtaani humo kabla kuhamishwa hadi katika hospitali ya rufaa ya Bungoma kwa matibabu zaidi. Aidha, alileza kuwa maafisa wake wameanza kumwinda bwana huyo.
‘’ Tumeanzisha msako mkali dhidi ya mshukiwa huyo na tutamfikisha kortini baada ya kumkamata,’’ alisema.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/28/kisa-cha-baba-aliyemchoma-bintiye-sehemu-nyeti-kwa-pasi/
No comments:
Post a Comment