Polisi wameanza uchunguzi kubaini chanzo cha mkasa huo. Picha: Hisani.
Polisi huyo aliandamana na walinzi wengine kusindikiza mabunda ya noti kwenye benki
Mlinzi huyo wa kike alijeruhiwa vibaya
Polisi wameanza uchunguzi kubaini chanzo cha mkasa huo
Kilizuka kioja katika mtaa wa Mlimani Nairobi huku afisa mmoja wa polisi aliyeandamana na walinzi wengine kuichomoa bunduki na kumfyatulia risasi mmoja wa walinzi hao.
Maafisa hao kama kawaida walikuwa wakisindikiza mabunda ya noti hadi benki wakishirikiana na walinzi hao.
Afisa huyo wa polisi aliyetambuliwa kama Hussein Ali mwenye nambari ya usajili 252481 alimpiga risasi mlinzi huyo wa kampuni ya SGA kimakosa walipokuwa wakipeleka pesa katika ATM eneo la Hurlingam, Kilimani.
Kulingana na aliyeshuhudia kisa hicho na kuomba jina lake libanwe, walisikia mlio wa risasi na kuondoka mbio kuponya maisha wakijua kilikuwa mkasa wa wizi wa mabavu.
Baadaye waligundua kuwa afisa huyo alimpiga risasi mwenzake waliokuwa naye kazi pamoja.
Mlinzi huyo wa kike aliyetambulika kama Lucy Njeri Kamau ambaye ni mfanyikazi katika kampuni ya ulinzi ya SGA alijeruhiwa paja na viganja vya mkono.
Kulingana na taarifa iliyoandikwa katika kituo cha polisi, Lucy alipelekwa katika hospitali ya Nairobi alikotibiwa. OCPD wa eneo hilo ameeleza kuwa waliweza kupata maganda ya risasi iliyotumika na kuthbitisha kuwa uchungunguzi umeanzishwa na maafisawa upelelezi kubaini chanzo cha mkasa huo.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/28/kioja-polisi-ampiga-risasi-mlinzi-wakisindikiza-pesa-benki-pamoja/
No comments:
Post a Comment