Monday, July 27, 2020

Lema: Sina imani kwa tabia nzuri waliyoonyesha jeshi la polisi ninaona ni kama chloroquine imepakwa sukari

Aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema amesema hana amani kwa tabia nzuri waliyoontesha jeshi la polisi jana wakati wa mapokezi ya Makakamu wa Chama cha Demokrasia (Chadema), Tundu Lissu.

Lema amesema anapaswa kujiuliza maswali mengi na majibu yawe tofauti na fikra za watu wengi.

“Ninaona ni kama chloroquine imepakwa sukari, kuna kitu kinafikiriwa na sisi tinapaswa kufikiri zaidi,” aliandika Lema katika ukurasa wake wa Twitter.

Lema aliandika ujumbe huu ” Sina amani kwa tabia nzuri waliyoonyesha jeshi la polisi jana wakati wa mapokezi ya Mh Tundu Lissu. Nina paswa kujiuliza maswali mengi na majibu yawe tofauti na fikra za watu wengi, ninaona ni kama chloroquine imepakwa sukari, kuna kitu kina fikiriwa na sisi tuna paswa kufikiriwa zaidi,”.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/28/lema-sina-imani-kwa-tabia-nzuri-waliyoonyesha-jeshi-la-polisi-ninaona-ni-kama-chloroquine-imepakwa-sukari/

No comments:

Post a Comment