Kaimu katibu mkuu wa Yanga Wakili Simon Patrick amesema naodha wa klabu hiyo Papy Tshishimbi amepewa siku 14 na klabu kusaini mkataba mpya au kuondoka ndani Yanga kwakua wapo wachezaji wengi wa aina yake.
Akizungumza na kituo cha redio cha Wasafi Fm Wakili Patrick amesema siku ya mwisho ya kurejesha mkataba aliokabidhiwa na timu hiyo ni Agosti 12, 2020.
“Mkataba wa Tshishimbi na Yanga SC unafikia kikomo 12/8/2020 na tumempa ofa ya mkataba mpya anaotakiwa kusaini ndani ya siku 14, endapo hatosaini basi tunamtakia kila la kheri kwani wachezaji kama yeye wapo wengi sana” amesema Wakili Patrick.
Mpaka sasa bado Papy hajasaini mkataba mpya na Yanga akidai timu hiyo haijampa ofa anayohitaji yeye.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/30/yanga-tayari-kuachana-na-tshishimbi/
No comments:
Post a Comment