Simon Murimi alikiri kumuua mpenziwe Eunice Wambui
Alieleza kuwa alimuua Eunice katika kijiji cha Kianderi, Kirinyaga Juni 23
Wakili wake aliimbia Mahakama hiyo kuwa Simon alimuua misichana huyo kumtoa kafara kwa ibada ya shetani
Mahakama kuu ya Kerugoya, Kenya imetoa adhabu ya kifungo cha miaka 30 gerezani kwa Simon Murimi, kijana aliyemuua mpenziwe Eunice Njeri Juni 23.
Akizungumza mbele ya hakimu katika Mahakama ya Kerugoya, Simon alikiri kumuua mpenziwe huyo katika kijiji cha Kianderi, Kirinyaga.
Simon alipewa adhabu ya kifungo cha miaka 30 gerezani. Picha: Hisani
Kupitia kwa wakili wake Magara Kemuntu, Simon aliiomba mahakama hiyo kumuonea huruma maana hakuwa ametenda kitendo kama hicho awali, kando na hivyo, alieleza kuwa hakumuua mpenziwe kwa kupenda bali aliagizwa kufanya hivyo na miungu.
Baada ya kumuua mpenziwe, aliuzika mwili wake katika shimo alilolichimba kama la takataka.
Baba alishuku kuhusu shimo hilo na keshowe akaamua kulichimbua, kwa mshangao, aliupata mwili ukiwa umezikwa mle ndani.
Maafisa wa polisi waliarifiwa kuhusu kisa hicho na kufika hapo upesi na kuufukua mwili huo huku Murimi akikamatwa na kuzuiliwa korokoni.
Inadaiwa kuwa Simon alijiunga na dini hilo la kigiza miaka michache iliyopita alipokuwa kazini mjini Mombasa.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/30/jamaa-aliyemuua-mpenzi-kumtoa-kafara-kwa-uabudu-shetani-afungwa-jela-miaka-30/
No comments:
Post a Comment