Friday, July 24, 2020

Kikwete asimulia alivyokwenda kumuona Rais Mstaafu Mkapa hospitali jana jioni

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete amesema jana alikwenda hospitali kumuona Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa, na hakuwa ni mgonjwa wa kumtilia shaka.

“Kifo ni siri ya mwenyezi Mungu jana jioni nilikwenda kumuona hospitali, hakuwa mgonjwa kwamba unatilia shaka, nimeondoka nikimuaga kwamba nitakuja kesho kukuona. kifo ni siri kubwa maanaake ungekuwa unajua ungeweza kusema hata tunaagana kabisa,” amesema Kikwete.amesema

Kikwete amesema tumempoteza mtu ambaye amelitumikia taifa vizuri , kwa heshima nauadilifu mkubwa.

“Tunaomba Watanzania katika kipindi hiki ni kuendelea na kuomboleza  kuwa na moyo wa subira kukubali tu kwamba kifo kimeumbwa na mwenyezi Mungu kila mmoja ndio njia yake,” alisema Kikwete

Rais Mstaafu Kikwete ambaye tayari ameshawasili kwenye nyumbani kwa marehemu na kusaini kitabu cha maombolezo.

Rais mstaafu Mkapa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa amelazwa hospitali kwa ajili ya matibabu jijini Dar es Salaam.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/24/kikwete-asimulia-alivyokwenda-kumuona-rais-mstaafu-mkapa-hospitali-jana-jioni/

No comments:

Post a Comment