Saturday, July 25, 2020

Heche awajia juu polisi sakata la kumpokea Lissu awaambia waifute Chadema ibaki CCM

Aliyekuwa Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche, amesema kila siku tatu wanakwenda viwanja vya ndege kuwapokea wageni wao.

“Hata wachezaji wa mpira wanapokelewa na mashabiki wao, wanamziki, familia zinapokea wapendwa wao kila siku,” aliandika Heche katika ukurasa wake wa Twitter.

“Kwanini polisi Tanzania mnaonyesha chuki na unaguzi mkubwa kiasi hiki kwa watu wa upinzani, futeni Chadema ibaki CCM,” aliandika Heche.

Jeshi la Polisi Nchini limetoa onyo kali kwa viongozi wanaohamasisha mikusanyiko ya watu isiyo zingatia sheria za nchi na yenye lengo ovu kwa taifa.

Kauli hii imetolewa leo Julai 25, 2020 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, kufuatia kuwepo kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA wanaohamasisha watu kupitia mitandao ya kijamii kukusanyika kwenda kumpokea mmoja wa wanachama wao anayetarajia kuwasili nchini Tanzania kwenye uwanaja wa Mwalimu Nyerere Julai 27, 2020.

Jeshi la polisi limesema linatambua watanzani wapo kwenye kipindi cha maombolezo lakini hilo halitawazuia kuwawajibisha kwa mujibu wa sheria wale wote wanaokusudia kufanya mikusanyiko bila kuzingatia sheria.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/25/heche-awajia-juu-polisi-sakata-la-kumpokea-lissu-awaambia-waifute-chadema-ibaki-ccm/

No comments:

Post a Comment