Thursday, July 30, 2020

Jamaa Apigwa Vibaya kwa kuwaagiza Abiria Kuvalia Barakoa

Man bitten by bus passenger he asked to wear face mask

Muphy alileza kuwa alipigwa kifuani na abiria huyo aliyekuwa na hasira mbaya. Picha: Hisani

Abiria huyo alikuwa ameketi na mkewe barakoa zao zikiwa chini ya mdomo

Virusi vya corona vimegeuza kabisa hali ya maisha, si kunawa mikono kila mara, si kujirashia sanitaiza, si kuvalia barokoa, yote ambayo watu hawakuzoea kabla ya mlipuko wa virusi hivyo.

Hatua hizi zote zimewekwa kama njia ya kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.

Robert Murphy, raia wa ubelgiji alijipata pabaya baada ya kuwashauri abiria wenza kuvalia vizuri barakoa baada ya kugundua kuwa barakoa yake ilishushwa chini ya domo.

Murphy ambaye alikuwa na majeraha kifuani alieleza kuwa abiria huyo ambaye alikuwa akisafiri pamoja na mkewe alimpiga vibaya mara mbili kifuani baada ya kumkumbusha kuvalia barakoa hiyo ipasavyo.

‘’Nilimwambia tu avalie barakoa vizuri. Alikataa na hapo vita vikazuka,’’ Murphy alisma.

Kulingana na Murphy mwenye umri wa miaka 56, alijaribu kujikwamua baada ya kukamatwa na bwana huyo lakini akashindwa kutokana na hali yake ya ulemavu.

The Right Mask for the Task - COVID-19 - Johns Hopkins Bloomberg ...

‘’Nilijaribu kujikwamua, lakini mimi ni mlemavu hivyo sikuweza.  Tulivutana hadi bwana huyo akajirusha kifuani mwangu na kuniumiza. Sikuamini. Alikuwa na hasira ya mbwa wazimu. Nilijaribu kumsukuma lakini akanikwamilia. Muda huo wote alitaka kuniuma tena.’’ Mzee huyo alisema.

Kwa mujibu wa Jarida la New York Post, abiria wengine waliingilia kati na kumuokoa Murphy huku jamaa huyo na mkewe wakiruka kutoka kwenye gari hilo.

Wawili hao walikamatwa na polisi baadaye  huku Murphy akifika hospitalini kwa matibabu.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/30/jamaa-apigwa-vibaya-kwa-kuwaagiza-abiria-kuvalia-barakoa/

No comments:

Post a Comment