Friday, July 24, 2020

Membe: Tutamkumbuka Rais Mstaafu Mkapa kwa akili kubwa ya uchambuzi

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amesema yeye na familia yake imeshtushwa na kusikitishwa sana na kifo cha ghafla cha Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.

“Tutamkumbuka kwa akili kubwa ya uchambuzi, uwezo wake wa kusuluhisha migogoro barani Afrika na uwanadiplomasia uliotukuka. Poleni wanafamilia RIP,” aliandika Membe  katika ukurasa wake wa Twitter.

Rais Mstaafu Mkapa amefariki usiku wa kuamkia leo akiwa amelazwa hospitali kwa ajili ya matibabu jijini Dar es Salaam.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/24/membe-tutamkumbuka-rais-mstaafu-mkapa-kwa-akili-kubwa-ya-uchambuzi/

No comments:

Post a Comment