Friday, July 24, 2020

Ubalozi wa Marekani umesema Rais Mstaafu Mkapa atakumbukwa kwa mengi ikiwemo amani na mageuzi ya uchumi

Ubalozi wa Marekani nchini umesema unaungana na Watanzania katika kuomboleza kifo cha Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa kilichotokea usiku wa kuamkia leo alipokuwa amelezwa katika hospitali kwa ajili ya matibabu jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ubalozi wa Marekani waliyoitoa leo kupitia ukurasa wake wa Twitter  umeeleza kuwa Mkapa alifanya kazi bila kuchoka kuleta amani na ustawi, sio tu kwa Tanzania bali kwa kanda yote.

“Jitihada zake za kuleta mageuzi katika uchumi, kupiga vita rushwa  na kupunguza kasi ya kuenea kwa VVU zitakuwa na matokeo makubwa chanya kwa Tanzania kwa vizazi vingi vijavyo. Mchango wake hautasahulika,” taarifa hiyo ilieleza



source http://www.bongoleo.com/2020/07/24/ubalozi-wa-marekani-umesema-rais-mstaafu-mkapa-atakumbukwa-kwa-mengi-ikiwemo-amani-na-mageuzi-ya-uchumi/

No comments:

Post a Comment