Tuesday, July 28, 2020

JPM Awasili Mtwara Tayari Kumzika Mkapa

ImageRasi wa Tanzania John Magufuli amewasili salama kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara tayari kwa ajili ya kushiriki mazishi ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa.

Rais Magufuli anataraji kuongoza wakazi wa kijiji cha Lupaso na mkoa wa Mtwara hapo kesho Julai 29, 2020 kumzika Rais huyo mstaaafu aliyefariki usiku wa kuamkia Julai 24, 2020 kutokana na maradhi ya moyo.

Mwili wa mzee Mkapa umewasilia wilayani Masasi leo baada ya kufanyika kwa shughuli ya kuagwa kitaifa kwenye uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam. 

Image



source http://www.bongoleo.com/2020/07/28/jpm-awasili-mtwara-tayari-kumzika-mkapa/

No comments:

Post a Comment