Monday, July 27, 2020

Mdee amelishukuru jeshi la polisi na kueleza wanawapenda

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kawe (Chadema), Halima Mdee, amelishukuru jeshi la polisi na kusema wanawapenda.

Amesema wasikubali maslahi ya watu wachache wakavuruga upendo na akili ya taifa letu.

Mdee ameandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter masaa machache baada ya kupokelewa Makamu wa Chama cha Demokrasia (Chadema), Tundu Lissu.

“Asanteni sana @tanpol !!! Tunawapenda sana!! Sisi ni watu wema!!! Tanzania ni yetu sote. Tusiruhusu maslahi ya watu wachache watuvurugie upendo wa asili wa taifa letu,” aliandika Mdee.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/28/mdee-amelishukuru-jeshi-la-polisi-na-kueleza-wanawapenda/

No comments:

Post a Comment