Sunday, July 26, 2020

Mnyika: Ratiba ya Lissu ipo pale pale tutampoke ni haki yetu

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, amesema ratiba ya ujio wa Makamuo wao Tundu Lissu haijabadilika.

Mnyika amesema Lissu atarejea kesho majira ya saa 7:20 mchana na watakwenda kumpokea.

“Kumpokea Airport DSM ni Uhuru wetu na haki yetu,” aliandika Mnyika katika ukurasa wake wa Twitter.

Mnyika amesema Lissu atakwenda kuaga mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa Julai 28, 2020.

“Mwenyezi Mungu atujalie tuwe na upendo, utu, haki, hekima, umoja na amani,” aliandika Mnyika



source http://www.bongoleo.com/2020/07/26/mnyika-ratiba-ya-lissu-ipo-pale-pale-tutampoke-ni-haki-yetu/

No comments:

Post a Comment