Friday, July 31, 2020

Waziri Kamwelwe amtumbua Meneja wa Tanroads

 

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, ametengua nafasi ya Meneje wa Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoa wa Lindi, Mhandisi Isack Mwanawima.

Waziri Kamwelwe ametoa taarifa hiyo jana kwa vyombo vyake habari kuhusiana na kumsimamisha kazi Meneja huyo.

Amesema jana Rais John Magufuli akiwa anatokea kijiji cha Lupaso katika mazishi ya Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, ameshuhudia ubovu mkubwa wa barabara kipande cha Nangurukuru hadi Mbwemkuru yenye urefu wa kilometa 90.

“Kwa kuwa nilishawahi kutoa maelekezo kwa mameneja wa mkoa wa Tanroads kuhakikisha barabara wanazosimamia zinakuwa kwenye hali nzuri na zinapitika,” taarifa hiyo ilieleza.

Amesema kutokana na uzaifu huo ametengua nafasi ya meneja huyo na kumuagiza Mtendaji Mkuu wa Tanroads apeleke mhandisi mwingine haraka kwa ajili ya kuimarisha usimamizi na kufanya maboresho ya Barbara hiyo.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/31/waziri-kamwelwe-amtumbua-meneja-wa-tanroads/

No comments:

Post a Comment