Sunday, July 26, 2020

Lisuu atupia video akielekea kupanda ndege

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ameonyesha picha ya video wakati akiende kupanda ndege.

Katika video hiyo Lissu aliongozana na mkewe, dereva wake wakiwa wanatembea kuelekea uwanja wa ndege kwa ajili ya kuanza safari jana usiku kuja Tanzania.

Lissu anaingia leo nchini majira ya saa 7:20 mchana na kesho anatarajia kwenda kumuaga Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.

Lissu aliondoka nchini miaka mitatu iliyopita kwa ajili ya kwenda kutibiwa nje ya nchi baada ya kushambuliwa kwa risasi akiwa anataka bungeni na watu wasiojulikana.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/lisuu-atupia-video-akielekea-kupanda-ndege/

No comments:

Post a Comment