Monday, July 27, 2020

Lissu Atuma Salama CCM “Tusindikizane Kumuaga Mkapa”

Image

Makamu mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu amesema kesho pamoja na wanachama wa chama hicho wataenda kwenye shughuli ya kitaifa ya kuaga mwili wa Rais msaafu Benjamin Mkapa.

Akizungumza baada yakufika makao makuu ya chama hicho jijini Dar es salaam Lissu pia ametoa pole kwa wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuondokewa na mwenyekiti wao wa zamani.

“Niwape pole wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuondokewa na M/Kiti wao wa zamani, huu msiba ni wetu sote, siyo wa Rais Magufuli pekee na kwa sababu ni msiba wetu sote, kesho Mungu akijalia basi tusindikizane tukampe Mkapa heshima yake ” amesema Lissu

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/lissu-atuma-salama-ccm-tusindikizane-kumuaga-mkapa/

No comments:

Post a Comment