Thursday, July 23, 2020

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Kaijage amebadilisha majina ya Majimbo matatu

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji  Semistocles Kaijage amebadilisha majimbo ya majina matatu.

Jaji Kaijage ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habarri kuhusiana na ratiba ya kuchukua fomu kwa ngazi ya urais, ubunge na udiwani.

Jimboa Chilonwa ambalo kwa sasa litaitwa Chamwino, jimbo la Mtera litaitwa Mvumi na jimbo la kijitopele lililopo wilaya ya Magharibi B litaitwa Pangawe.

Aidha, Jaji Kaijage ametangaza ratiba ya kuchukua na kurejesha fomu kwa nafasi ya urais, ubunge na udiwani.

Amesema kwa nafasi ya urais fomu zitaanza kutolewa kuanzia Agosti 5 hadi 25, 2020 jijini Dar es Salaam na fomu za ubunge na udiwani zitatolewa kuanzia Agosti 12 hadi 25, 2020.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/23/mwenyekiti-wa-tume-ya-uchaguzi-jaji-kaijage-amebadilisha-majina-majimbo-matatu/

No comments:

Post a Comment