Aina hiyo ya nyani (Mountain gorillas) ni nadra mno. Picha:Hisani
Felix Byamukama alikiri kumuua nyani huyo
Alileza kuwa nyani huyo alimvamia ndipo akaamua kumuua kama njia ya kujikinga
Bwana mmoja raia wa Uganda atalazimika kutumikia kifungo cha miaka 11 jela baada ya kupatikana na hatia kwa kumuua nyani kinyume cha sheria.
Akizungumza mbele ya hakimu, Felix Byamukama alikiri kuingia kwenye mbuga la wanyama na kumuua nyani huyo aliyetambulika kama Rafiki.
Byamukama alidai kuwa alimuua Rafiki kama njia ya kujikinga baada ya nyani huyo kumvamia mbugani humo. Kando na hivyo, alikiri kuingia kwenye mbuga hilo la Bwindi kwa lengo la kuwawinda wanyama wadogo na wala si kwa nia ya kumuua nyani huyo.
Uchunguzi ulibaini kuwa Rafiki alifariki kutokana na kudungwa sehemu za ndani kwa kifaa chenye makali.
Nyani huyo alitoweka Juni 1, na mwili wake kupatikana siku moja baadaye. Picha: Hisani
Kwa mujijibu wa jarida la BBC, maafisa ya UWA, kitengo kinachosimamia wanyama pori walimtafuta muuaji huyo na kumpata kijijini akiwa na silaha za uwindaji.
Nyani huyo anadhaniwa na kuwa na umri wa miaka 25,akiwa ni aina moja ya nyani ambayo huwa nadra sana.
Rafiki alikuwa rafiki mkuu wa wanadamu na kila watalii walipofika mbugani, aliwapa upendo mkubwa kwa kutangamana nao na kutembea nao kila mahali.
Inadaiwa kuwa mwindaji huyo alipoingia mbugani, huenda nyani huyo alidhania ni mtalii na kama kawaida alitaka kutangamana naye na katika hali hiyo akauliwa.
Mbuga zimefungwa kwa muda tangu kulipuka kwa virusi vya corona.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/31/jamaa-aliyemuua-nyani-uganda-afungwa-miaka-11-gerezani/
No comments:
Post a Comment