Monday, July 27, 2020

Familia Yafunguka Kuhusu Kilichomuua Mzee Benjamin Mkapa

Great friend, outstanding': Uhuru, Raila mourn Benjamin Mkapa

Mzee Mkapa alifariki akiwa na umri wa miaka 81. Picha: Hisani

Familia ya aliyekuwa Rais wa muungano wa jamuhuri ya Tanzania Mzee Benjamin Mkapa imefunguka kuhusu chanzo cha kifo chake.

Familia hiyo imefutilia mbali uvumi kuwa Mkapa alifariki kutokana na virusi vya corona na kueleza kuwa alikuwa akiugua malaria lakini akafa kutokana na mshtuko wa moyo.

Mkapa ambaye alihudumu kama Rais wa awamu ya tatu wa Muungano wa Jamuhuri ya Tanzania alifariki Ijumaa, Julai 24 mjini Da es Salaam akiwa na umri wa miaka 81.

Kifo cha kiongozi huyo kilitangazwa na Rais John Pombe Magufuli licha ya kukimya kuhusu chanzo cha kifo chake.

‘’ Mkapa alipatakana na Malaria na akalazwa kwa matibabu tangu Jumatano’’ William Erio alisema kama ilivyopeperushwa na runinga ya TBC1 Jumapili, Julai 27.

Opinion: Magufuli′s COVID-19 apathy is a recipe for disaster ...

Kifo cha Mzee Mkapa kilitangazwa na Rais John Pombe Magufuli. Picha: Hisani

Erio ambaye ni jamaa ya hayati alieleza kuwa kiongozi huyo ambaye alikuwa Rais tangu 1995-2005 alikuwa na nafuu Alhamisi kiasi cha kutazama habari kwenye runinga. Hata hivyo alibainisha kuwa Mkapa alifariki kutokana na mshtuko wa moyo siku moja baadaye.

Viongozi wa Afrika walilimwaya kumuomboleza Mkapa kwa kutuma salamu za rambirabi kwa jamaa na marafiki wa hayati wakimrundia sifa kwa juhudi zake katika kuipigisha hatua kubwa Tanzania na kudumisha Amani Afrika Mashariki.

Rais wa muungano wa jamuhuri ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli aliwaongoza Watanzania katika kumuomboleza Mzee Mkapa.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/familia-yafunguka-kuhusu-kilichomuua-mzee-benjamin-mkapa/

No comments:

Post a Comment