Sunday, July 26, 2020

Lissu Atua Ethiopia

Tanzanian Opposition Leader Tundu Lissu - YouTubeMakamu mwenyekiti wa chama ha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu ameendeela na safari ya kuanza kurejea nyumbani Tanzania ikiwa ni baada ya takribani miaka mitatu ya kukaa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Lissu ambaye alitangaza uamuzi sa kurejea nchini mapema wiki iliyopita ametuma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter na kusema amefika salama nchini Ethiopia tayari  kuunganisha ndege ya kutua nchini.

“Nimetua salama uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole hapa Addis Ababa, nasubiri kuunganisha ndege kuja nyumbani” ameandika Lissu.

Kwa mujibu wa taarifa aliyotia awali makamu huyo mwenyekiti anatarajia kutua nchini Leo Julai 27, 2020 majira ya saa saba mchana.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/lissu-atua-ethiopia/

No comments:

Post a Comment