Monday, July 27, 2020

Mwili wa Rais Mstaafu Mkapa umewasili uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuagwa

Mwili wa marehemu Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa umeshafika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa.

Rais John Magufuli ataongoza viongozi wa ndani na nje ya nchi kuaga mwili wa Rais Mstaafu Mkapa.

Baada ya kukamilika kwa taratibu za kuaga mwili huo utasafirishwa kupelekwa jijini kwake Lupaso kwa ajili ya maziko.

Usiku wa kuamkia Ijumaa Julai 24, 2020 Rais Mstaafu Mkapa alifariki akiwa amelazwa hospitali kwa ajili ya matibabu jijini Dar es Salaam.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/28/mwili-wa-rais-mstaafu-mkapa-umewasili-uwanja-wa-uhuru-kwa-ajili-ya-kuagwa/

No comments:

Post a Comment