Aliyewahi kuwa rais wa chama cha wanansheria Tanganyika (TLS) Fatma Karume amehoji ni kwa nini Uchaguzi mkuu visiwani zanziba ufanyike ilhali shirika la utangazaji nchini (TBC) limentaja Dkt Hussen Mwinyi kuwa rais mteule wa Zanzibar.
Karume amehoji hayo kupitia ujumbe alituma lwenye ukurasa wa twitter na kuongeza kuwa kitendo cha kumtanga Mwinyi kama rais mteule ni kuvunja katiba.
“Kama Hussein ni Rais Mteule wa Zanzibar ya nini kupiga kura Oct 2020. Si wamtangaze tu? Wanasubiri nini? Kipindi cha Shein kimalizike? Wanaheshimu kipindi kilicjowekwa na katiba yetu? Kama Katiba yetu haiheshimiwi na tunabandikizwa Rais mteule basi wamuapishe tu” ameandika Fatma Karume.
Dkt Hussein Mwinyi ameteuliwa na mkutabo mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) manamo Julai 10,2020 jijini Dodoma kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi Oktoba.
Kama Hussein ni Rais Mteule wa #Zanzibar ya nini kupiga KURA Oct 2020. Si wamtangaze tu? Wanasubiri nini? Kipindi cha Shein kimalizike? Wanaheshimu kipindi kilicjowekwa na KATIBA yetu? Kama Katiba yetu haiheshimiwi na tunabandikizwa RAIS MTEULE basi wamuapishe tu! https://t.co/34r1pIz5jB
— fatma karume aka Shangazi (@fatma_karume) July 29, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/07/29/fatma-karume-ahoji-zanzibar-kupiga-kura-wakati-rais-ameanza-kutangazwa/
No comments:
Post a Comment