Alidai kuwa mumewe alikuwa mnyonge kitandani. Picha: Hisani
Aliwavamia wawili hao kwa hasira
Alishuku wawili hao walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kulingana na jinsi mkewe alivyokuwa akimtunza mlinzi huyo
Mamia walikusanyika kutazama sinema hiyo
Ilitokea sinema ya bure katika mtaa wa South B huku mume akimfumania mlinzi wa lango lake akihusika katika tendo la ndoa na mkewe kwenye kitanda chake cha ndoa.
Jamaa huyo alichukua hatua ya kumchunguza mkewe baada ya kuona jinsi alivyokuwa akimtunza mlinzi huyo.
Siku ya kisa, jamaa huyo alitoka kuenda kazini lakini akarudi muda mfupi baadaye, alinyatanyata akafungua mlango baada ya kumkosa mlinzi huyo langoni, akampata wakilishana uroda kitandani.
Bwana huyo alizua fujo na kumpiga mlinzi huyo kwa hasira swala lililowavutia majirani na wapiti njia.
Mlinzi huyo alilazima kufunguka baada ya kupata mapigo mazito, alieleza kuwa mama huyo alikuwa akimlipa ili kumtoshelezea mahitaji ya kimwili.
Kwa uande mwingine, mwanamke huyo alidai kuwa mumewe alikuwa mnyonge kitandani na ndiyo maana aliamua kutafuta mtu wa kuweza kumsaidia.
Ilibainika kuwa wawili hao walikuwa na tofauti za kinyumbani na kwa muda hawakuwa wakizungumziana.
Aidha, mama huyo alidai kuwa mumewe hakuwa anakila chakula chake kwa muda huku mumewe akimlaumu kuwa mlevi kupindukia.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/30/mwanamke-amlaumu-mumewe-baada-ya-kufumaniwa-na-mlinzi-kitandani/
No comments:
Post a Comment