Wednesday, July 29, 2020

Mwinyi: Nilivaa viatu siku niliyoenda Jandoni

Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi amesema yeye ni mkubwa kuliko wote kwani amezaliwa mwaka 1925.

Mwinyi ameyasema hayo leo wakati wa ibada ya mazishi ya Rais Mstaafu wa tatu, Benjamin Mkapa aliyezikwa jijini kwake Lupaso mkoani Mtwara.

Amesema ameshangaa kuona watu wamevaa vitu kwani yeye alivaa mara mbili ya kwanza akiwa anakwenda jandoni.

“Nimevaa viatu mara mbili mara ya kwanza nilipoenda jandoni na mara ya pili nikiwa na miaka 13 nilichuma karafuu nikapata hela nikanunua viatu,” amesema Mwinyi.

Aliongezea “Viatu vyenyewe nilikuwa naviweka begani nikitembea ili visiishe,”.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/29/mwinyi-nilivaa-viatu-siku-niliyoenda-jandoni/

No comments:

Post a Comment