Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, amesema kuna nyakati ngumu na nzito alizokuwa anazipitia na nguzo yake alikuwa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.
“Alikuwa ni mmoja wa nguzo zangu za kuegemea katika kipindi kile kigumu kwa hiyo ni mtu aliyekuwa na msaada mkubwa,” amesema Kikwete.
Aidha, Kikwete amesema Mkapa alikuwa kiongozi mzuri, mzalendo na alikuwa na mapenzk makubwa na wananchi wa Tanzania.
Amesema alikuwa anachukia mazingira ya watu kuwa maskini, hivyo suala la uchumi alilipa kipaumbele.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/29/kikwete-kuna-kipindi-nilipita-nyakati-ngumu-mkapa-alikuwa-ni-nguzo-yangu/
No comments:
Post a Comment