Rais John Magufuli amewataka wafanyabiashara kwenye soko la Kibiti mkoani Pwani kuacha kulipa ushuru kwa uongozi wa soko hilo kutokana na kukosekana kwa huduma ya choo.
Rais Magufuli amesema hayo leo Julai 39,2020 aliposimama kuongea na wafanyabiashara wa wilaya hiyo akiwa njiani kurejea jijini Dar es salaam akitoka Mtwara kwenye mazishi ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.
“Natoa wiki moja DC na DED jengeni vyoo hapa, wafanyabiashara kuanzia leo msilipe ushuru hadi wajenge vyoo na kwa sasa tumieni vyoo vyao” amesema Rais Magufuli.
Rais JPM ameagiza Wakazi wa Kibiti kujisaidia kwenye vyoo wanavyotumia DC na DED wa Kibiti majumbani mwao kufuatia soko la Kibiti kukosa choo. “natoa wiki moja DC na DED jengeni vyoo hapa, wafanyabiashara kuanzia leo msilipe ushuru hadi wajenge vyoo na kwa sasa tumieni vyoo vyao” pic.twitter.com/jWcMbNTjMw
— millardayo (@millardayo) July 30, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/07/30/magufuli-awakataza-wafanyabiashara-kibiti-kulipa-ushuru/
No comments:
Post a Comment