Rais wa John Magufuli amesema aliongea na Rais wa awamu ya tatu hayati Benjamin Mkapa siku chache akiwa hospitalini kabla ya kifo chake Usiku wa kuamkia Julai 24,2020.
Rais Magufuli amesema alipoongea na hayati Mkapa alimtoa wasiwasi na kumuambia asijali na yupo salama.
“Mzee Mkapa niliongea nae akiwa Hospitalini kwa simu akaniambia ‘John usiwe na wasiwasi naendelea vizuri’ sikujua kuwa maneno yake yalikuwa ni ya kuniaga, namshukuru Mungu kazi ameikamilisha.. Mkapa, Mwinyi,Kikwete mara nyingi tunakuwa nao pamoja leo Mkapa hayupo”
Mwili wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa unatarajiwa kusafirishwa leo kwenda kijijini kwao Lupaso mkoani Mtwara kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Julai 29,2020.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/28/rais-magufuli-afunguka-kauli-ya-mwisho-aliyombiwa-na-mzee-mkapa/
No comments:
Post a Comment