Tuesday, July 28, 2020

Sonko Adai Kugundua Dawa Ya Corona

Sonko's Automated Sanitization Booths Vandalized And Puts Blame On ...Gavana wa jimbo la Nairobi, nchini Kenya Mike Sonko amesema amefanikiwa kupata tiba ya virusi vya Corona ambayo itamaliza tatizo la ugonjwa wa huo ulioua takribani watu milioni 1 duniani kote.

Sonko amesema moja kati ya ndugu zake walipata gonjwa hilo na walipona baada ya kupata dawa ambayo yeye ameigundua na kudai kuwa atangaza siku ya kuanza kutoa dawa hiyo kwa wananchi wa kawaida ya Nairobi na kenya kwa ujumla.

“Hii ni sababu kwa nini Mkenya yoyote hatakiwi kufariki kwa virusi hivi, kuna njia nimetumia kuweza kutibu virusi hivi na nimefanikiwa kuna mpwa wangu amepona kwa kutumia mbinu hizi nilizovumbua na baadhi ya dawa ambazo nimeshajua” amesema Sonko.

Sonko ameongeza kuwa ataitangaza rasmi dawa hiyo pindi atapo pata taarifa ya kuithishwa matumizi ya dawa hiyo kutokakwenye ofisi ya mganga mkuu wa nchi hiyo.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/28/sonko-adai-kugundua-dawa-ya-corona/

No comments:

Post a Comment