Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume amesema alilalamika kuhusu jengo lake kupigwa bomu na hakuna majibu yoyote aliyopewa hadi sasa.
Jana jeshi la polisi limemtaka mtu yoyote ambaye anahofu na usalama wake kutoa taarifa hizo polii ili ziweze kufanyiwa kazi badala ya kulalamika mitandaoni na kwenye vyombo vya habari vya ndani na nje.
“Mimi nimelalamika kuhusu jengo langu kupigwa bomu. Nimeenda mpaka kwa DCI pale HQ Wizara ya ndani @ tanpol mpaka hii leo hamjanipa majibu yoyote,” aliandika Fatma katika ukurasa wake wa twitter
“Bado mnataka nikae kimya ili iweje? nitalalamika tu kwamba hamjanipatia majibu yeyote wala hamjakamata mtu. tusitishane kabisa,”
Mimi nimelalamika kuhusu jengo langu KUPIGWA BOMU. Nimeenda mpaka kwa DCI pale HQ Wizara ya Ndani. @tanpol mpaka hii leo hamjanipa majibu yeyote. Bado mnataka nikae KIMYA? Ili iweje? Nitalalamika tu kwamba hamjanipatia MAJIBU yeyote wala hamjamkamata mtu. Tusitishane kabisa! https://t.co/2nbPkTbLyv
— fatma karume aka Shangazi (@fatma_karume) July 31, 2020
Fatma aliendelea kusema kuwa “Eti mpige mabomu majengo ya watu mpige risasi wenzake, mchoma visu wenzake, mtekaji na @tanpol wanaoshindwa kuwakamata si wachafu nchi, alkini sisi Victims tunaolalamika eti tunaichafua nchi? wekeni sheria ya kufunga walalamikaji badala ya wahalifu msitufanye wapumbavu,”.
Eti mpiga mabomu majengo ya watu; mpiga risasi wenzake; mchoma visu wenzake; mtekaji; na @tanpol wanaoshindwa kuwakamata si WACHAFUWA NCHI, lakini sisi VICTIMS tunaolalamina eti TUNAICHAFUWA NCHI? Wekeni sheria ya kufunga WALALAMIKAJI badala ya WAHALIFU! Msitufanye WAPUMBAVU!
— fatma karume aka Shangazi (@fatma_karume) July 31, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/07/31/fatma-karume-amelicharua-jeshi-la-polisi-na-kuwaambia-tusitishane-kabisa/
No comments:
Post a Comment