Msemaji mkuu wa serikali Dkt Hassani Abbasi amesema serikali itaifanyia kazi hoja ya kubadilisha jina ka uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kwa kupewa jina la Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam wakati akitoa utaratibu utakao tumia kesho kwa ajili ya shughuli ya kitaifa ya kuaga mwili wa Rais huyo mstaafu aliyefariki usiku wa kumkia Julai 24,2020 Dkt Hassani amesema ni hoja nzuri.
“Ni hoja nzuri tutaichukua kwa sasa acha tukamilishe shughuli za mazishi baada ya hapo mengine tutajua yatakuwaje maan wengi mnafahamu juu ya historia ya uwanja huu ambao tulipewa msaada na serikali ya China lakini serikali chini yake ilichangia pakubwa sana” amesema Dkt Abbasi.
Uwanja wa michezo wa taifa jijini Dar es salaam ukizunduliwa rasmi mwaka 2007 baada ya takribani miaka minne ya ujenzi wa uwanja huo wenye hadhi ya kimataifa.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/serikali-yatoa-majibu-hoja-kubadili-jina-uwanja-wa-taifa/
No comments:
Post a Comment