Rais John Magufuli amemteua,Luteni Kanali Patrick Kenani Sawala, kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.
Rais Magufuli amefanya maamuzi hayo leo baada ya kukutana na madudu wakati akirejea Dar es Salaam.
Luteni Kanali Sawala anachukua nafasi ya Juma Njwayo ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Uteuzi wa Luteni Kanali Sawala unaanza leo Julai 30, 2020.
Leo Rais Magufuli amewataka wafanyabiashara kwenye soko la Kibiti mkoani Pwani kuacha kulipa ushuru kwa uongozi wa soko hilo kutokana na kukosekana kwa huduma ya choo.
Rais Magufuli amesema hayo leo Julai 39,2020 aliposimama kuongea na wafanyabiashara wa wilaya hiyo akiwa njiani kurejea jijini Dar es salaam akitoka Mtwara kwenye mazishi ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa.
“Natoa wiki moja DC na DED jengeni vyoo hapa, wafanyabiashara kuanzia leo msilipe ushuru hadi wajenge vyoo na kwa sasa tumieni vyoo vyao” amesema Rais Magufuli.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/30/rais-magufuli-amtumbua-mkuu-wa-wilaya-rufuji-amteua-mrithi-wake/
No comments:
Post a Comment