Monday, July 27, 2020

Lissu: Mguu wa kulia umejaa vyuma na kuna risasi imeshindikana kutolewa ipo chini ya mgongo

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, amesema mguu wake umejazwa vyuma kwenye goti hadi kwenye nyonga pamoja na mkono wake wa kushoto hali ambayo imesababisha kushindwa kunyooka.

Lissu ambaye ni Makamu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema mbali na vyuma hivyo kuna risasi imeachwa ambayo ipo chini ya mgongo.

“Huu mguu wangu wa kulia umejaa vyuma kuanzia kwenye goti hadi kwenye nyonga vingine vipo kwenye mkono wa kushoto haunyooki, kuna risasi ipo iko chini ya mgongo  madaktari walisema ibaki hapo hapo ni salama zaidi kuliko kuitoa,” amesema Lissu.

Lissu amerejea leo kutoka nje ya nchi ambapo alikuwa akipatiwa matibabu katika kipindi cha miaka mitatu baada ya kushambuliwa kwa zaidi ya risasi 16 na watu wasiojulikana akiwa anatokea bungeni kuelekea nyumbani kwake mkoani Dodoma.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/lissu-mguu-wa-kulia-umejaa-vyuma-na-kuna-risasi-imeshindikana-kutolewa-ipo-chini-ya-mgongo/

No comments:

Post a Comment