Friday, July 31, 2020

Rais wa Gambia Atiwa Karantini, Naibu Wake Apatikana na COVID19

Adama Barrow: Gambia haitojiondoa ICC

Adama atajitenga humo kwa wiki mbili. Picha: Hisani

Rais wa Gambia Adama Barrow ameingizwa karantini baada ya naibu wake kupatikana na virusi vya corona

Kulingana na taarifa ya ikulu, Adama atajitenga humo kwa wiki mbili

Virusi vya corona vimezidi kuunguza mataifa bila huruma hata baada ya masharti makali kuwekwa kama njia ya kujikinga.

Virusi hivyo vikitekeza bila kujali tabaka, hali na mali, viongozi wa mataifa mbali mbali wameambukizwa virusi hivyo bila kuwaacha wananchi wa kawaida.

Awamu hii, virusi hivyo vimetikisa Gambia. Rais wa nchi hiyo Adama Barrow akichukua hatua ya kujitenga kwenye karantini baada ya naibu wake kupatikana na virusi hivyo hatari.

Kwa mujibu wa ikulu ya nchi hiyo, Barrow atasali karantini kwa wiki mbili huku madaktari wake wakimchunguza kwa karibu.

Rais huyo aliamua kujitia karantini baada ya kutangamana na naibu wake ambaye pia alipatikana na virusi hivyo.

Hadi sasa, Gambia imerekodi vsa 326 vya maambukiza ya corona pamoja na vifo nane.

Serikali imesisitiza kuhusu kufuatwa kwa kanuni za wizara ya afya katika kujikinga na virusi hiyo hatari.

Kwingineko, mkewe Rais wa Brazil Michelle Bolsanaro pia amethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.

Kulingana na vyombo vya habari nchini humo, Michelle alipatikana na virusi vya corona Julai 30, siku moja tu baada ya kuhudhuria mkutano wa hadhara akiandamana na mumewe.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/31/rais-wa-gambia-atiwa-karantini-naibu-wake-apatikana-na-covid19/

No comments:

Post a Comment