Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema mwili wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa hautawasiri kwenye uwanja wa ndege wilayani Nachingwea kama ilivyotangazwa hapo awali.
Akizungumza na wanahabari kwenye kijiji cha Lupaso ambako Rais mstaafu Mkapa anatarajiwa kuzikwa Julai 29,2020 amesema msafara utakao beba mwili huo utafikia moja kwa moja kijijini hapo.
Mkuu huyo wa mkoa huyo ameongeza kuwa msafara utakaobeba mwili wa mzee Mkapa utapokelewa kijijni hapo Julai 28, 2020 majira ya jioni baada ya kumalizika kwa shughuli za kuaga kitaifa jijini Dar es salaam.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/mabadiliko-ratiba-msiba-wa-mkapa/
No comments:
Post a Comment