Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, amesema Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wanamuombea kwa mwenyezi Mungu kama kuna makosa ambayo aliyafanya aweze kusamehewa.
Amesema ni mwanadamu kama ilivyo binadamu wengine pengine katika umri wake aliwahi kuteleza akafanya kosa asilolipenda Muumba wetu aweze kumsamehe.
‘Mwenzenu akiondoka jambo la kwanza ni kumuombea msamaha kwa mwenye Mungu endapo amekosea Mwenyezi Mungu amsameehe amuwie radhi na hiyo ni moja ya mafundisho ya dini yetu tuliyofundishwa,” amesema Mwinyi.
“Hivi leo nasimama hapa kutoa rambirambi kwa mama Mkapa na watoto na kwa watu wote pamoja na mkoa huu kwa kuondokewa na rafiki mpenzi,”
Amesema marehemu Mkapa alikuwa ni mtu mzuri na mwema na pia ni mfanyakazi hodari hana utani katika kazi.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/29/mwinyi-tunamuombea-msamaha-mkapa-kwa-mwenyezi-mungu-kama-kuna-sehemu-aliteleza-asamehewe/
No comments:
Post a Comment