Wahudumu hao wa afya wanaofanya maziko wameeleza kuhusu kuambukizwa msongo wa moyo
Wengi huamini kuwa wameambukizwa covid19 na hivyo wanaisambaza kwa wasiojua
Wameeleza kuwa marafiki wao wamewatema
Wahudumu afya waliojitolea kuhakikisha wanasaidia katika maziko ya watu waliaangamia kutokana na virusi vya corona kama njia ya kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo sasa wamelilia kile walichokitaja kama ubaguzi.
Maafisa hao wanadai kuwa tangu walipoanza kuhusika katika kazi hiyo ya maziko, wengi katika jamii hawataki kutengamana nao tena wakiwataja kama wagonjwa wa virusi hivyo hatari vya corona wenye uwezo mkubwa wa kuwaambukiza virusi hivyo.
Mlipuko wa virusi vya corona vimebadilisha utamaduni wa kuzika miili, shughuli hiyo ikiachiwa wahudumu wa afya tu haswa kwa wale wanadhaniwa kuambukizwa.
Maziko ya kifahari hayapo tena, mwili hutajika kuzikwa chini ya masaa 24 baada ya kufariki kuzuia usambazaji wa virusi hivyo. Picha: Hisani
Caleb Kipsang’ na Violet Pember ambao ni wahudumu wa afya wanaojihusisha na shughuli hiyo ya maziko wameeleza kuwa wamepoteza marafiki tangu walipoanza kazi hiyo inayaoambatanishwa na maambukizi ya virusi vya covid19.
‘’Wanapokuona, wanakuona kama virusi. Unawapoteza marafiki wa karibu, hata kukutana haiwezekani,’’ Kipsang.
‘’ Hata wenzetu kazini. Ukikutana na mtu , anasonga mbali. Hamwezi kutangamana na kuzungumza tena,’’ Violet.
Kulingana na wizara ya afya, miili ya watu waliofariki kutokana na virusi vya corona inapaswa kuzikwa kati ya 7am na 9am.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/maafisa-wa-afya-wa-kuzika-miili-ya-waliongamia-na-covid19-wazua-malalamishi/
No comments:
Post a Comment