Kulingana naye, babake alimpa Tsh 2000 ili asimtaje katika kisa hicho. Picha: Hisani
Jamaa Amnajisi Mwanawe wa Miaka 6 Kabla Kumkimbiza Hospitalini
Alimpa mtoto huyo Tsh 2000 ili kusema kuwa alidungwa na kijiti alipokuwa akicheza
Mtoto huyo alieleza kisa kamili kilichojiri baada ya madakatari kumhoji kwa muda
Alikuwa na maumivu makali
Wanasema kuishi kwingi kuona mengi, Madaktari wa hospitali ya rufaa ya Hola wamesalia kwa mshngao baada ya jamaa moja kumleta mwanawe wa miaka sita hospitalini humo kuapata matibabu baada ya kumnajisi.
Kwa mujibu wa jarida la Nation, mtoto huyo alidai kuwa alidungwa sehemu nyeti na kijiti alichokuwa akikichezea.
Visa vya ubakaji vimekithiri. Picha: Hisani
Baada ya madaktari kufanya uchunguzi wa kina, ilibainika kuwa mtoto huyo alinajisiwa. Walifanya kila nia kumshawishi mtoto huyo aeleza kuhusu kilichojiri.
Msichana huyo aliwaacha wengi vinywa wazi akieleza kuwa babake wa kumzaa alimnajisi na kumleta hospitalini humo alipolalamikia maumivu makali.
‘’Aliletwa akiwa hajiwezi, alikuwa amepoteza damu kupita kiasi na alikuwa na maumivu makali. Tulifanya tuwezavyo kabbla kumhoji,’’ daktari alisema.
Kulingana naye, babake alimpa Tsh 2000 ili asimtaje katika kisa hicho.
Msichana huyo anaendelea kupata matibabu katika hospitali hiyo ya rufaa ya Hola huku babake akizuiliwa na polisi kusubiri kufunguliwa mashtaka.
Wengi wamesalia wajiuliza alichofikiri bwana huyo kiasi cha kumgeukia mwanawe wa kuzaa na kumbaka.
Visa vya wazazi kuwanajisi na kuwadhulumu wanao vimepanda chanzo kikikosa kujulikana.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/30/jamaa-amnajisi-mwanawe-wa-miaka-6-kabla-kumkimbiza-hospitalini-kwa-matibabu/
No comments:
Post a Comment