Tuesday, July 28, 2020

Si Covid 19, Rais Yowero Museveni Aeleza  Alivyoambukizwa Ugonjwa kwa Kuvaa Barakoa

Yoweri K. Museveni.

Rais Yoweri Museveni alikuwa na shida ya koo, mojawapo ya dalili za virusi vya covid19

Aliwaita madaktari wake kumfanyia vipimo vya covid19

Alieleza kuwa alikuwa akitumia tangawizi, ndimu na asali lakini dalili hizo hazikuisha

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amejitokeza na kubaini kuwa hali yake i shwari kuhusiana na maambukizi ya virusi vya corona.

Rais huyo alieleza kuwa alipatwa na hofu baada ya kuonyesha dalili za virusi hivyo akiwa na shida ya koo swala lilomfanya kuchukua hatua ya kuwaita madaktari wake kumfanyia vipimo vya virusi vya covid.

Akizungumza muda mfupi baada ya chama chake kumteua kama mgombezi wa urais katika uchaguzi wa 2021, Museveni aliomba msamaha kutokana na hali ya sauti yake na kubaini kuhusu kisa kizima.

‘’ Naomba msamaha kwa sauti isiyo ya kawaida. Jumamapili nilianza kuwa na shida ya koo na kitu cha kwanza nlichofikiria ni corona, niliwaita madaktari, walifanya vipimo na jioni walipoleta matokeo, yalionyesha sina virusi hivyo,’’ alisema.

Kulingana na Museveni, madaktari hao walithibitisha kuwa alikuwa na maambukizi ya bakteria ambayo yalisababishwa na uvaaji wa barakoa wakati wa kuzungumza.

‘’ Nimekuwa nikitumia tangawizi, ndimu na asali na sasa sauti itakuwa sawa,’’ aliongezea.

Hadi Jumanne, Agosti 28, Uganda ilikuwa imerekodi visa vya maambukizi ,135 wote wakiwa maraia wa nchi hiyo.

Hadi mwezi Juni, Rais huyo alieleza kuwa alichukua hatua ya kuwakataza zaidi ya watu 1,067 walioambukizwa virusi vya corona waliotaka kuingia nchini humo.

Wizara ya afya ilithibitisha kisa cha kwanza cha mtu aliyefariki kutokana na virusi hivyo Julai 21 nchini humo.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/29/si-covid-19-rais-yowero-museveni-aeleza-alivyoambukizwa-ugonjwa-kwa-kuvaa-barakoa/

No comments:

Post a Comment