Friday, July 24, 2020

Kituo cha Redio Chafungwa, Baada ya Wanahabari 9 Kuambukizwa Covid19

List of Radio Stations in Kenya and Their Frequencies in 2019 ...

Wote walipatwa na virusi hivyo ila mmoja tu. Picha: Hisani

Mfanyikazi mmoja wa kituo hicho alipatikana na virusi vya corona

Wengine wote walienda hospitalini kufanyiwa vipimo baada ya kutangamana naye

Wote walipatwa na virusi hivyo ila mmoja tu

Kituo hicho kilifungwa kusubiri kupulizwa dawa

Kituo cha Redio cha Redio Light and Life kilichoko Kericho Kenya, kilifungwa Alhamisi , Julai 23 baada ya wafanyikazi tisa wa kituo hicho kupatikana na virusi vya corona.

Mtu wa kwanza alifanyiwa vipimo Jumatatu, Julai 20 na kutiwa karantini katika kituo cha hospitali ya rufaa ya Kericho baada ya kupatikana na virusi hivyo.

Katika taarifa iliyotiwa saini na kiongozi wa kituo hicho,  Lyton Yegon, wafanjyikazi wengine wa redio hiyo walifanyiwa vipimo baadaye na kupatikana na virusi hivyo.

LIGHT AND LIFE MEDIA LIMITEDOFFICIAL STATEMENT ON COVID 19 EFFECT ON THE ORGANISATIONGood AfternoonWe would like to…

Posted by Radio Light and Life 107.3 Fm- Changing Lives on Thursday, 23 July 2020

‘’ Wafanyikazi wote tisa wametiwa karantini na shuguli ya kutafuta waliotangamana nao inafanyiwa na idara ya afya, kaunti ya Kericho,’’ taarifa hiyo.

Kulingana na Yegon, wafanyikazi wote wa kituo hicho waliambukizwa virusi ila mmoja tu.

Aidha, alitangaza kuwa kituo hicho kitafungwa kwa muda wa wiki mbili kutoa nafasi ya kunyunyiziwa dawa.

‘’ Tumezungumza na wakurugenzi, Media council pamoja idara ya afya, kaunti ya Kericho iliamua kufunga kituo hicho kwa wiki mbili,’’ alileza.

Wizara ya afya imewashukuru pakubwa watu waliojitokeza na kutangaza wazi kuwa waliambukizwa virusi vya corona, hiyo ikiwa njia ya kuhamasisha umma zaidi kuhusu hatari ya virusi hivyo.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/24/kituo-cha-redio-chafungwa-baada-ya-wanahabari-9-kuambukizwa-covid19/

No comments:

Post a Comment