Mikel Arteta. Picha: Hisani
Arsenal imepiga hatua kubwa tangu Mike Arteta aliposhika usukani
Klabu hiyo imefuzu kwa fainali za FA
Arteta yuko njiani kuirejesha Arsenal alikoiacha Wenger
Klabu ya Arsenal imeweza kupanda na kupata utukufu wake wa zamani chini ya kiongozi Mike Arteta.
Licha ya meneja huyu kudai kuwa klabu hiyo haijafika anapotaka kuifikisha, Arsenal imeonekana kungaa tena kama zamani ilivyokuwa chini ya Wenger.
Arteta ameweza kuisukuma klabu hiyo na kuhakikisha inafuzi kwa fainali za FA, kilichosalia ni mageuzi machache anayonuia kuifanyia klabu hiyo.
Kulingana naye, wachezaji wengi wa klabu hiyo tayari wana umri mkubwa na wengine kukosa kasi.
Arteta ameutaka usimamizi wa klabu hiyo kuwasaka wachezaji wapya wa kiongo cha mashamabulizi, kiungo cha kati na walinzi.
Mesut Ozil. Picha: Hisani
Huku nafasi ya uhamisho ukiwa wazi wachezaji wawili wa Arsenal Mesut Ozil na Guendozi wako kwenye orodha wachezaji wa timu hiyo watakaonyeshwa njia ya kuondoka
Tangu alipochukua usukini Mike Arteta, Mesut Ozil ameshiriki mechi chache sana. Hata baada ya kueleza kwa yuko tayari kwa mechi dhidi ya Liverpol, Arteta hakumpa nafasi mchezaji huyo.
Guendozi. Picha: Hisani
Kwa upande mwingine, Guendozi ambaye katu hakukosa nafasi Unai Emerry alipokuwa kiongozi wa klabi hiyo vile vile amekuwa kwenye jamvi kwa muda mrefu tangu Arteta alipoingia.
Habari zilizovuja zinaeleza kuwa mchezaji huyo atauzwa ili kumsaini nyota wa Barcelona Counthino.
source http://www.bongoleo.com/2020/07/30/nyota-2-wa-arsenal-kuonyeshwa-mlango-baada-ya-kutofautiana-na-arteta/
No comments:
Post a Comment