Mamii ya watu wajitokeza kumpokea Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) , Tundu Lissu, kwenye uwanja wa ndege wa Terminal III jijini Dar es Salaam.
Wananchi hao wakiwa na shauku ya kumuona Lissu wengine walikuwa wamepiga magoti katika foleni waliyopanga eneo ambalo wanatokea wasafiri.
Lissu anatarajia kushuka wakati wowoto kuanzia sasa aliwa anatokea nje ya nchi alipokuwa anapatiwa matibabu katika kipindi cha miaka mitatu.
Lissu alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 16 na watu wasiojulikana akiwa anatokea bungeni kuelekea nyumbani kwake.
Watu waliojitokeza kumpokea @TunduALissu wakiwa Terminal 3 Uwanja wa J.K Nyerere, eneo la kusubiria watu wanaowasili. Muda mfupi kuanzia sasa, Tundu Lissu atalakiwa.#LissuArejeaTanzania pic.twitter.com/QuFpdZt8MJ
— EastAfricaRadio (@earadiofm) July 27, 2020
source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/mamia-ya-watu-wafurika-kumpokea-lissu/
No comments:
Post a Comment