Saturday, July 25, 2020

Uchimbaji wa kaburi la Rais Mstaafu Mkapa ukiendelea

Shughuli ya kuandaa kaburi inaendelea katika eneo la makaburi ya familia nyumbani kwao na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu marehemu Benjamin Mkapa jijini Lupaso Wikaya ya Masasi mkoani Mtwara.

Rais Mstaafu Mkapa ataagwa kwa mfululizo wa siku tatu kuanzia Julai 26 hadi 28 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na atazikwa Julai 29, 2020 kijijini kwake.

Rais Mstaafu Mkapa alifariki usiku wa kuamkia jana akiwa amelazwa hospitali kwa ajili ya matibabu jijini Dar es Salaam.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/25/uchimbaji-wa-kaburi-la-rais-mstaafu-mkapa-ukiendelea/

No comments:

Post a Comment