Friday, July 31, 2020

Mbwa wa Kwanza aliyepatikana na COVID19 Afariki Amerika

Buddy: First dog to test positive for COVID-19 in the US dies

Buddy alipatakana na corona Mei 2020 baada ya kuanza kuugua tangu Aprili 2020

Indaiwa kuwa mbwa huyo aliambukizwa virusi hivyo na mmiliki wake

Mmiliki huyo alieleza kuwa mbya huyo alianza kudhoofika na kutapika damu iliyoganda

Mbwa aina ya German Shepard mwenye umri wa miaka saba aliyekuwa wa knwa kupatikana na virusi vya covid19 amefariki, New York.

Mbwa huyo aliyepewa jina Buddy alifariki Jumamosi, Julai 11 baada ya kuugua kwa miezi mitatu.

Kulingana jarida la CNN, madaktari wa mifigo waliochunguza ripoti ya mbwa huyo walielza kuwa alikuwa akiugua saratani.

‘’ Haibainiki iwapo saratani ilimfanya kuambukizwa kwa urahisi na virusi vya corona, ama huenda ilikuwa ni sadfa tu.

Mbwa huyo alianza kuugua Aprili 2020, mmiliki wake Robert Mahomey alimshuku kuambukizwa virusi vya corona, alipomuita daktari wa mifugo, alifanya vipimo na kuthibitishwa kuwa kweli alikuwa na virusi hivyo.

Juni, 2, 2020, kitengo cha kilimo USDA kilithibitisha kuwa Buddy alikuwa mbwa wa kwanza kuambukizwa covid19.

USDA hadi sasa imethibitisha idadi ya takriban mbwa 12 na paka 10 walioambukizwa corona.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/31/mbwa-wa-kwanza-aliyepatikana-na-covid19-afariki-amerika/

No comments:

Post a Comment