Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.
Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.
Zinazobamba leo ni pamoja na jinsi maelfu walivyomuaga Mkapa, Makamu wa Rais apata Corona na mwisho ni juu ya Mtia nia ashitakiwa kwa kusambaza picha za ngono. Karibu
MAELFU WAMZIKA MKAPA
KIJIJI cha Lupaso, Kata ya Lupaso wilayani Masasi mkoani Mtwara, jana kilizizima kutokana na wingi wa watu waliojitokeza kushiriki maziko ya Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa.
Maelfu ya wananchi walijitokeza katika kijiji hicho jana bila kujali jua, vumbi na umbali kutoka maeneo yao kwenda kuaga mwili wa kiongozi huyo.
MAKAMU WA RAIS APATA CORONA
Makamu wa Rais wa Gambia, Isatou Touray amekutwa na maambukizi ya COVID19 na kutokana na hilo, Rais Adama Barrow atajitenga kwa muda wa siku 14
Taarifa iliyotolewa na Serikali haikuelezea kwa undani kuhusu hali ya kiafya ya Touray (65) ambaye alitangazwa kuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo mwaka jana
Soma zaidi>>>
ASHITAKIWA KWA PICHA ZA NGONO
MSANII na Ofisa Masoko wa Clouds, Mwemba Burton maarufu Mwijako (35), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka ya kusambaza picha za ngono kupitia mtandao wa WhatsApp.
Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka yake jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate.
Upande wa Jamhuri uliongozwa na Mawakili wa Serikali Waandamizi, Wankyo Simon na Mwanaamina Kombakono.
Kombakono alidai kuwa kati ya Septamba 17 na Oktoba 10, 2019, mshtakiwa alisambaza picha za ngono kupitia mtandao wa WhatsApp.
Soma zaid>>>
source http://www.bongoleo.com/2020/07/30/dondoo-za-leo-maelfu-walivyo-mzika-mkapa-makamu-wa-rais-apata-corona-ashitakiwa-kwa-kutuma-picha-za-ngono/
No comments:
Post a Comment