Friday, July 24, 2020

Wanandoa Wajawa Furaha Kuruhusiwa Kumpa Mwanao Jina Shetani (Lucifer)

Dan Sheldon and his baby, Lucifer

Wanandoa hao marai wa New Zealand wamewasha mitandao baada ya kumpa mwanao jina Lucifer

Dan na Mandy Sheldon walikataliwa awali kuhusu jina hilo kabla kupeleka malalimishi yao kortini

Hatimaye waliruhusiwa kulitumia jina hilo

Wanasema kuzaa si kazi kazi ni kulea mwana, lakini je umewahi kuwaza kuhusu kibarua cha kumpa yule mwana jina, Au je, jina huchangia vipi katika malezi na tabia ya mtoto baadaye.

Wanandoa maraia wa New Zealand wameewaacha wengi kwa mshangao mkubwa na kuiwasha mitandao baada ya kuwasilisha kesi mahakamani wakitaka idhini ya kumpa mwanao jina Lucifer, jina linalotumiwa kumtaja shetani.

Dan na Mandy Sheldon hawakuchoka hata baada ya kukataliwa kutumia jina hilo kwa mwanao alipozaliwa wakionywa kuwa hueda likamletea mtoto huyo changamoto baadaye.

‘’Alituonya kuwa mtoto huyo hatapata kazi , na walimu hawatataka kumfundisha. Nilijaribu kumuelezea kuwa sisi si watu wa kidini na kuwa neno Lucifer humaanisha mleta mwanga, na asubuhi kiugiriki. Alidinda kuelewa,’’ Dan alisema.

‘’Alituambia ni hatia kumpa mtoto jina Lucifer nchini New Zealand. Alitushauri tumpe mtoto huyo jina jingine lakini tukiwa nyumbani tunaweza kumuita Lucifer,’’ aliongezea.

Walipiga hatua nyingine hadi katika mahakama kuruhusiwa kutumia jina hilo, na baada ya miezi minne, mahakama ikawapa idhini na kuwapa raha kubwa kumpa mwano jina wapendalo.

Habari kuhusu jina hili limezua mjadala mkali mitandaoni, wengi wakishangaa ni kwanini mtu anaweza kuamua kumpa mwanwe jina kama hili ilhali yapo majina mengi ya kuweza kutumika.



source http://www.bongoleo.com/2020/07/24/wanandoa-wajawa-furaha-kuruhusiwa-kumpa-mwanao-jina-shetani-lucifer/

No comments:

Post a Comment