Monday, July 27, 2020

Amkata Mapanga Binti Wa Miaka 16 Kwa Kukataa Kuolewa

Chopped handsPolisi katika eneo la Bududa kwenye kaunti ndogo ya Nakatai nchini Uganda wanachunguza juu ya kisa cha msichana wa miaka 16 kukatwa mkono na mguu na anyedai kuwa mpenzi wake baada ya kukataa ombi lake la kumuoa.

Binti huyo ambaye yupo nyumbani akiendelea kupona majeraha yake amekatwa mkono wa kulia na mguu wa kushoto na mpezi wake huyo aliyemshambulia kwa panga siku kadhaa zilizopita akiwa nyumbani kwa wazazi wake majira ya usiku.

“Alitaka kunioa lakini nilikata ombi lake kwa sababu nataka niendele na masomo lakini hakupokea vizuri taarifa yangu” amenukuliwa binti huyo na mtandao wa NairobiNews.

Binti ameongeza kuwa mbali na kukatwa mkono pia amejuruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake na panga alilokuwa ameshika mtuhumiwa huyo ambaye alikamatwa na kuachiwa na polisi wa eneo hilo kwa mujibu wa taarifa za wazazi wa binti huyo.

 



source http://www.bongoleo.com/2020/07/27/amkata-mapanga-binti-wa-miaka-16-kwa-kukataa-kuolewa/

No comments:

Post a Comment